September 4, 2020 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro amewasili Kisiwani Pemba kwa ajili ya kufanya vikao na Vyama vya Siasa, Viongozi wa dini lengo kufanya Uchaguzi Mkuu kwa amani na salama.
“Ndoto yetu sisi Polisi tutende haki ili tuwe na uchaguzi wa amani, Pemba nimekuja kuongea na Kamati za Ulinzi na Usalama, Viongozi wa dini na Viongozi wa Siasa tukubaliane maana wote ni sehemu ya Uchaguzi, nitatoa elimu na kuna wengine nitawapa elimu lakini hawatoifuata” IGP Sirro