Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, amesema kuwa wamejipanga kulinda amani katika kipindi zoezi la upigaji kura kwenye uchaguzi Mkuu huku akitaja sababu kwanini wameweka askari wakutosha mkoani Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkoani Arusha, Sirro amewaambia wananchi kuwa askari wamejipanga kuhakikisha wanasimamia amani na haki.
“Arusha ni mahala ambapo miaka ya nyuma kulitokea fujo kwahiyo ni mahala ambapo tumepanga, tumeweka askari wa kutosha, askari wa kirai, wa operesheni na askari wa upepelezi wote wapo timamu kuhakikisha arusha inakuwa shwari” IGP Sirro
“Nina taarifa kuna vikundi vichache vinataka kuleta uvunjifu wa amani wasijaribu kufanya hivyo wakifanya hivyo maana yake wanajiingiza kwenye kutenda makosa natutawashugulikia kabla ya siku yenyewe” IGP Sirro