Rais wa Israel Isaac Herzog alionekana mwenye msimamo katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mjini Jerusalem.
Alisema kuwa Israel haitaki vita vya Hezbollah lakini akaongeza kuwa Lebanon ‘italipa gharama’ ikiwa Hezbollah itaiingiza Israel kwenye vita.
“Nadhani dola ya uovu ya Irani inawaunga mkono na inafanya kazi siku baada ya siku kuharibu Mashariki ya Kati na kanda. Ninataka kuweka wazi – hatutafuti makabiliano kwenye mpaka wetu wa kaskazini na mtu mwingine yeyote.
Tumelenga kuharibu miundombinu ya Hamas na kuwarudisha raia wetu nyumbani,” Rais wa Israel alisema.
“Lakini kama Hezbollah itatuingiza kwenye vita, inapaswa kuwa wazi kwamba Lebanon italipa gharama ,Lebanon haiwezi kuwa mwanachama huru wa jumuiya ya kimataifa, raia wake hubeba pasipoti ya Lebanon, lakini inapokuja kwa Israeli hawawajibiki … .
Kwa sheria za kimataifa, tuna haki kamili ya kujitetea.”