Uchunguzi wa awali wa “poda nyeupe” iliyopatikana katika Ikulu ya Marekani limeripotiwa kuwa ni madawa ya cocaine, mamlaka ya utekelezaji wa sheria ilisema huku Mamlaka ya Secret Service ya Marekani ikichunguza mapema wiki hii jinsi madawa hayo yalipatikana kwenye jengo hilo.
Kupatikana kwa madawa ya kulevya aina ya “cocaine” ambayo yametumwa kwenye maabara kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi kujulikana wakati timu ya zima moto na timu ya vifaa vya hatari ya idara ya moto ya Washington DC ilipotangaza kuwa wamepata “cocaine hydrochloride,” gazeti la Washington Post liliripoti.
Msemaji wa Idara ya “Secret Service” ya MArekani Anthony Guglielmi aliiambia Washington Post kwamba ugunduzi huo ulisababisha hali ya taharuki na kama njia ya tahadhari watu walihamishwa kutoka kwenye jengo hilokwa lengo la kuimarisha usalama. Ripoti za awali zilionyesha kuwa madawa haya yailigunduliwa katika maktaba ya marejeleo. Shirika la habari la Associated Press, likiwanukuu maafisa wawili ambao hawakuidhinishwa kuzungumza juu ya uchunguzi huo, baadaye Jumanne liliripoti kwamba unga huo mweupe ulipatikana “katika eneo linalofikiwa na vikundi vya watalii, sio katika ofisi yoyote ya West Wing”.
Wakati wa ugunduzi huo Rais Joe Biden alikuwa mapumzikoni Camp David akiwa na mke wake Jill Biden jijini Maryland na kurejea Ikulu ya Marekani asubuhi ya jana. Afisa mwenye ufahamu kuhusu uchunguzi huo aliliambia gazeti la Washington post kuwa madawa yaliyopatikana yalikuwa kwa kiasi kidogo. Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa madawa ya kulevya kuingia Ikulu kwani Rapa Snoop Dogg alisema kuwa alivuta bangi ndani ya maliwato ya ikulu mwaka 2013.