Kuna taarifa imenifikia leo kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kanda na Kimataifa kuhusu ishu mbili, kwanza kuhusu oparesheni ya kukamata wahamiaji haramu na pia ishu ya agizo la kupiga marufuku mavazi ya vimini.
Majibu yaliyotolewa leo ni kwamba Serikali inahimiza watu kuvaa mavazi ya heshima lakini Rais Magufuli hajapiga marufuku mavazi ya aina yoyote ikiwemo sketi fupi.
Kwa upande wa wafanyabiashara wageni, Serikali imesema kuna oparesheni ya kawaida ya kukamata wahamiaji haramu wasio na vibali, hiyo haihusiani na wala haimaanishi kuwafukuza wafanyabiashara wageni.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE