Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wanne Ikulu, Dar es salaam.
Taarifa kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa alisema Rais Magufuli alikuwa na na mazungumzo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Juma Assad kuhusu kupunguza gharama za matumizi ya kuendesha serikali na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Prof. Assad ameagizwa pia na Rais Magufuli kuhakikisha Tanzania inaongeza ukusanyaji wa mapato kutoka 14% ya pato la Taifa.
Rais Magufuli pia amekutana na Mkurugenzi wa Mashitaka Tanzania, (DPP) Biswalo Eutropius Mganga ambaye amesema mazungumzo yao yalihusiana na mikakati ya namna ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka inavyopaswa kufanya kazi ili kuendana na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano isemayo “Hapa Kazi Tu”.
Kiongozi Mwingine aliyekutana na Rais Magufuli ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuber Ally ambaye amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE