Serikali ya Luxemburg imetangaza rasmi kuruhusu kilimo cha bangi na matumizi ya bangi ambapo hatua hii inaifanya Nchi hii iwe Nchi ya kwanza kwenye Bara la Ulaya kuruhusu kilimo cha bangi pamoja na matumizi yake ambapo chini ya sheria hii mpya, Watu wazima wenye zaidi ya miaka 18 wataruhusiwa kutumia bangi na kuotesha hadi mimea minne kwa kila nyumba.
Hata hivyo bado kutumia bangi hadharani itabaki kuwa haramu ndani ya Taifa hilo, vilevile kwenye upande mwingine mbegu za biashara pia zinaruhusiwa chini ya sheria mpya bila kikomo kwa kiwango au viwango vya Tetrahydrocannabinol (THC), sehemu ya kisaikolojia ya bangi.
Luxemburg ambayo ni miongoni mwa Nchi kumi tajiri duniani inatajwa kuwa miongoni mwa Nchi zinazojali zaidi Watu wake ambapo vingine vilivyoruhusiwa ni usafiri wa Mabasi na Treni kuwa bure kwa Watu wote iwe ni Raia au asiye Raia.