Halima Msabaha ni Mama wa miaka 62 mkazi wa Mbezi DSM, anayeishi kwenye nyumba ambayo imebomoka yeye pamoja na Mtoto wake ambaye ni mlemavu, anasumbuliwa na maradhi kutokana na mshtuko alioupata baada ya nyumba kubomoka hasa ukizingatia hana kipato kwa sasa na Familia inamtegemea, nyumba aliijenga kwa fedha za mirathi alizopata baada ya Mumewe kufariki.
“Mwanangu ni mlemavu wa akili, amejitoboa pia macho yote mawili kwa sindano, nateseka Ndugu zangu wananiita mchawi, naambiwa nihame sina pa kuhamia”–Halima
Namba za kuwasiliana na Halima ni 0683602120 na 0677819697.