Club ya wekundu wa Msimbazi Simba leo Jumatatu ya August 28 2017 kupitia taarifa iliyotolewa na afisa habari wake Haji Manara inaeleza kuwa golikipa wao Said Mohamed Nduda amepata jeraha la goti na hivyo atapelekwa nje ya nchi kutibiwa.
Saidi Mohamed Nduda kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na afisa habari wa Simba Haji Manara, inaeleza kuwa Nduda aliumia wakati wa maandalizi ya mchezo wa Ngao ya hisani kati ya Simba dhidi ya Yanga, kutoka na uchunguzi kufanyika, Nduda sasa atasafirishwa kwenda kutibiwa India.
Golikipa huyu atasafiri mwishoni mwa wiki hii kuelekea India na atakuwa nje ya uwanja kwa wiki nne hadi saita, hata hivyo John Bocco na Haruna Niyonzima aliyeumiwa juzi, wameanza mazoezi na wenzao leo wakati Shomari Kapombe ambaye ni majeruhi wa muda mrefu ataanza mazoezi hivi karibuni.
Video ya dakika 2 ikionyesha Hat-Trick ya Okwi iliyookoa Milioni 5