India imewatambulisha marubani wanne wa Jeshi la Anga ambao wameorodheshwa kusafiri kwa chombo cha kwanza cha anga ya juu mwaka ujao.
Ujumbe wa Gaganyaan unalenga kutuma wanaanga watatu kwenye obiti ya kilomita 400 na kuwarudisha baada ya siku tatu.
Shirika la anga za juu la India Isro limekuwa likifanya majaribio kadhaa kujiandaa na safari ya ndege hiyo.
Mnamo mwenzi Oktoba, mwaka janajaribio kuu la safari hiyo lilionyesha kuwa wafanyakazi wanaweza kukwepa kwa haraka na salama iwapo roketi itaharibika
Baada ya mafanikio yake, Isro alisema ndege ya majaribio ingechukua roboti angani mnamo 2024, kabla ya wanaanga kutumwa angani mnamo 2025.
Katika hafla iliyofanyika katika kituo cha Isro katika mji wa kusini wa Thiruvananthapuram (zamani ukiitwa Trivandrum) siku ya Jumanne, wanaanga hao wanne walielezewa kama “wenye ndoto, wasafiri na wanaume mashujaa wanaojiandaa kwenda angani”.