Rais Samia Suluhu amesema India ina kila sababu ya kuwa mwekezaji namba moja nchini Tanzania na si wa tatu au tano kutokana na ushirikiano baina ya nchi hizi mbili na historia inayoziunganisha.
Rais Samia ameyasema hayo leo wakati akizungumza katika Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na India lililofanyika jijini New Delhi, India ikiwa sehemu ya ziara yake ya kitaifa ya siku nne nchini India.
Aidha Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TCCIA) Angelina Ngalula, amesema ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini India imefungua milango ya ushirikiano kati ya pande zote mbili.
Amesema tayari mazungumzo yamefanyika. Mbali na uingizaji wa mitaji kutoka nje, kuna makubaliano ya kubadilishana taarifa za kibiashara na ujuzi kuhusu fursa za biashara zinazoweza kuzalishwa kati ya nchi hizi mbili.