Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amejitolea kuisaidia Ukraine katika juhudi za kuleta amani, Modi ameyasema haya wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Ukraije Volodymyr Zelenskiy.
Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali, India iko tayari kuchangia kwa njia yoyote kuelekea juhudi za amani wakati Rais Zelenskiy alipomweleza kuhusu hali ya mgogoro nchini Ukraine.
Siku ya Ijumaa, India, China na Falme za Kiarabu walijizuia kupiga kura kwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukataa uvamizi wa Urusi, hatua iliyosababisha ukosoaji mkubwa kutoka nchi za Magharibi na kupokea sifa kutoka kwa Urusi ambayo wamekuwa kwa muda mrefu na mahusiano ya ulinzi.
India imetuma vikosi maalum nchini Poland, Hungary na Romania kwenda kuwahamisha Raia wake kupitia Nchi hiyo jirani na Ukraine.