India inajiandaa kurusha roketi yake mwezini siku ya Jumatano, wakati wa kihistoria kwa nchi hiyo yenye watu wengi zaidi duniani ambayo inatarajia kujiunga na klabu ya kipekee ya wale waliofanikiwa kutua mwezini, miaka minne baada ya jaribio kama hilo kushindwa.
Chandrayaan-3 inatarajiwa kutua mwezini muda mfupi baada ya saa kumi na mbili jioni saa za India (sawa na nusu sa za Afrika ya Kati), karibu na ncha ya kusini ya mwezi, yaani upande wa giza wa Mwezi, ambao haujagunduliwa sana, jambo ambalo litakuwa la kwanza ulimwenguni kwa programu ya anga.
Hii ni sehemu ya mwezi ambapo hakuna chombo chochote ambacho kimewahi kufanikiwa kutua.
Jaribio hili jipya la programu ya India, kwa kasi kamili, linakuja miaka minne baada ya jaribio lingine kama hili kushindwa vibaya, timu ya iliyokuwa ardhini ilipoteza mawasiliano muda mfupi kabla ya kuwasili mwezini.
Chandrayaan-3 iliyotengenezwa na Shirika la Utafiti wa Anga la India (ISRO), inajumuisha moduli ya kutua iitwayo Vikram, inayomaanisha “shujaa” kwa Kisanskrit, na roboti ya rununu, inayoitwa Pragyan (“hekima” kwa Kisanskrit) ili kuchunguza uso wa Mwezi.
Misheni hii inafanyika siku chache baada ya Luna-25, kifaa cha kwanza kuzinduliwa na Urusi kwenda mwezini tangu mwaka 1976, kuanguka.
Chandrayaan-3, iliyozinduliwa wiki sita zilizopita, ilikwenda kwa mwendo wa kinyonga kufikia mwezini kuliko misheni ya Apollo ya Marekani ya miaka ya 1960 na 1970, ambayo ilifika mwezini kwa siku chache.