Mara nyingi wazazi hushauriwa kuona umuhimu wa kukuza vipaji vya watoto wao tangu wakiwa wadogo, taarifa ikufikie kuwa mtoto mwenye umri wa miaka miwili ameweka rekodi nchini India kutokana na uwezo wake wa kulenga shabaha ya mishale.
Kutokana na vitabu vya kumbukumbu vya rekodi za taifa hilo, mtoto huyo Dolly Shivani Cherukuri, ameweka rekodi ya kuwa mshiriki mwenye umri mdogo zaidi kupata alama 200, katika mashindano yaliyofanyika wiki iliyopita.
Jarida la Press Trust la India, limesema mtoto huyo alirusha mishale 36 kutoka umbali wa mita 5 na mita 7 na kupata alama 388, tukio lililoshuhudiwa na wachezaji wakongwe na maafisa kutoka idara ya kumbukumbu za michezo.
Baba yake Cherukuri Satyanarayana ambae ni mmiliki wa club moja inayofundisha kurusha mishale amesema, alimfundisha kurusha mishale tangu alipozaliwa, kwa sasa ana mpango wa kumpeleka kushiriki katika mashindano ili afikie hatua ya kuingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness.
Mcheki kwenye hii video hapa…
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>>twitter Insta Facebook