India inakuwa nchi yenye watu wengi zaidi duniani kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, huku ikitajwa kuipita nchi ya China ikiwa na watu milioni 142.86 huku China yenyewe ikitajwa Kuwa na idadi ya watu milioni 142.57.
Kulingana na Kituo cha Utafiti cha Pew, idadi ya watu nchini India imeongezeka kwa zaidi ya watu bilioni moja tangu 1950, mwaka ambao UN ilianza kukusanya data ya idadi ya watu.
Beijing ilimaliza “sera yake kali ya mtoto mmoja”, iliyowekwa katika miaka ya 1980 kutokana na hofu ya ongezeko la watu, mwaka 2016 na kuanza kuruhusu wanandoa kupata watoto tatu mwaka 2021.
Uchina inakabiliwa na kupungua kwa idadi ya watu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1960 huku viwango vya kuzaliwa vikipungua na umri wa wafanyikazi wake kulishuhudiwa kushuka.
Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, idadi ya watu duniani itakuwa imefikia bilioni 8.045 kufikia katikati ya 2023.
Katika Afrika pia, mwelekeo wa ongezeko la watu unaweza kuonekana na inakadiriwa kuwa bara la pili kwa ukubwa ulimwenguni litashuhudia ongezeko la idadi ya watu kutoka kwa wakaazi bilioni 1.4 hadi 3.9 ifikapo 2100.
Mataifa manane yenye zaidi ya wakazi milioni 10, wengi wao wakiwa Ulaya, yaliona idadi yao ikipungua katika muongo mmoja uliopita.
Japani pia inaona kupungua kwa sababu ya watu wake kuzeeka, na kupoteza zaidi ya wakaazi milioni tatu kati ya 2011 na 2021.
Idadi ya watu katika sayari nzima, wakati huo huo, inatarajiwa kupungua tu katika miaka ya 2090, baada ya kilele cha bilioni 10.4, UN imekadiria.