Marina Smith Mtangazaji maarufu kutoka Brazil amedai kwamba amezuiwa kusherehekea Krismasi na Marafiki zake kwa sababu ya uzuri wake, Smith mwenye umri wa miaka 34 na mshindi wa Taji la Miss Bumbum alisema kwamba Wanawake wenzake walijawa na wivu na walihofia kuwa uzuri wake ungeweza kuvutia Waume na Wapenzi wao pia alisema, “Ndio, mimi ni Mwanamke mrembo, lakini hiyo si sababu ya kunitenga.”
Katika mahojiano na kipindi cha NeedToKnow, Smith alifunguka kuhusu hali hiyo akisema kuwa Marafiki zake walikuwa na wasiwasi kwamba angeweza kuvutia Wapenzi wao huku akiongeza kuwa yeye haji kwa nia ya kuvunja uhusiano wa Watu bali anapenda kuvaa mavazi yanayomfanya ajisikie vizuri.
Ukiachana na Smithi pia Sabrina Low, influencer mwenye umri wa miaka 23 naye alikumbana na hali kama hiyo alipozuiwa kutoka kwenye sherehe ya harusi ya Rafiki yake kwa sababu ya mwonekano wake.
Kwa Smith, hali hii inamuumiza zaidi kwa sababu anahisi kutengwa zaidi kutoka kwenye mikusanyiko ya Marafiki ambao ni wapenzi, alisema “Kuwa single tayari kunanifanya niishi maisha ya kijamii yenye ukomo, kwani Marafiki zangu mara nyingi hutoka na Wapenzi wao Sasa, kuwa single na Mrembo kumegeuka kuwa chanzo cha wivu kwao.”
Smith alisisitiza kuwa hata ingawa mara nyingi hujivunia sura yake kwa mavazi ya kisasa, lengo lake halikuwa kuvutia umakini au kuvunja uhusiano wa wenzake. “Tatizo si mimi,” alisema.