Nyota wa YouTube amefungwa jela miezi sita kwa kuangusha ndege yake kimakusudi ili kupata idadi kubwa ya watazamaji , na kisha kuwadanganya wachunguzi wa Marekani.
Trevor Jacob, 30, alichapisha video ya ajali ya ndege ndege iliyoonekana kuanguka mnamo Desemba 2021, akimaanisha kuwa ilikuwa ajali.
Alijiondoa kwenye ndege akiwa anajipiga picha ya selfie kwa kutumia kamera ya selfie ya fimbo na kuruka kwa kutumia parachuti kutoka kwenye ndege hadi akutua chini.
Klipu hiyo ilitazamwa mara milioni.
Katika makubaliano ya kuomba msamaha , Jacob alisema alirekodi video hiyo kama sehemu ya mpango wa udhamini wa bidhaa.
Mwanariadha huyo wa zamani wa Olimpiki alikiri hatia ya ulaghai huo mapema mwaka huu kwa kosa moja la uharibifu na kuficha kwa nia ya kuzuia uchunguzi wa shirikisho.
Jacob “uwezekano mkubwa alitenda kosa hili ili kutengeneza mitandao ya kijamii na matangazo ya habari kwa ajili yake mwenyewe na kupata faida ya kifedha,” waendesha mashtaka wa serikali ya California walisema Jumatatu.
Wiki chache baada ya tukio hilo, wachunguzi kutoka Bodi ya Kitaifa ya Usalama wa Anga na Utawala wa Shirikisho la Usafiri wa Anga (FAA) walianzisha uchunguzi katika ajali hiyo na Jacob aliamriwa kuhifadhi mabaki ya ndege hiyo ikijumuisha video zote. Youtuber huyo aliwaambia maafisa kuwa hajui ni wapi ndege hiyo ilianguka.