Moja ya story ambayo ina-make headlines kwenye mitandao siku za hivi karibuni ni pamoja na hatua ya Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kulifungia kwa miezi 24 Gazeti la kila wiki la Mawio.
Kutokana na tukio hilo wanaharakati wamepinga tukio hilo na miongoni mwao ni Jukwaa la Wahariri Tanzania ‘TEF’ ambao wamelaani ambapo leo June 20, 2017 Jukwaa hilo limetoa tamko juu ya hatua ya Waziri Mwakyembe kulifungia gazeti hilo wakisema amekiuka Sheria ya Huduma za Habari ya 2016 kwa kujivika mamlaka ya kimahakama ambayo kimsingi hana wajibu wa sheria hiyo.
FULL VIDEO: Rais JPM alivyotembelea Mkoa wa Pwani leo