Ilikuwa ni mshikemshike mkubwa pindi Hyatt Regency hoteli ambayo zamani ilijulikana kama Kilimanjaro Kempinsky ya jijini Dar es Salaam kutangaza ofa ya chumba cha milioni 22 na laki 4 kwa ajili ya Siku ya Wapendanao yaani Valentines Day.
Inaelezwa kuwa chumba hiki ni kile wanacholala marais pindi wakija nchini na kwa siku za kawaida bei yake huwa ni Dola za Marekani 5000 sawa na Tsh Milioni 11 za Kitanzania.
AyoTV na millardayo.com tumempata Meneja wa Hotel ambaye ametoa ufafanuzi kuhusiana na chumba na ameelezea ni huduma zipi mtu atazipata akiwa hapo.
TOP 10: HIZI NDIZO HOTELI ZENYE VYUMBA VYA BEI ZA JUU ZAIDI DUNIANI