Leo April 9, 2019 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro amewaonya wale watakao andamana bila ya kuwa na kibali watakuwa wanatenda uhalifu.
Sirro ametoa onyo hilo wakati kukiwa na taarifa kwenye mitandao kijamii juu ya kufanyia kwa maandamano ya amani Mkoani Dodoma yanayoratibiwa na kijana anaedaiwa kutoka chama Cha ACT-Wazalendo.