Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya kisiasa nchini haina uhalisia kwa kuwa mazingira ya kisiasa yako vizuri.
Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa ilitoa taarifa juu ya Haki za Binadamu na kuonesha wasiwasi wake juu ya hali ya Tanzania.
Profesa Kabudi amesema kuwa tathmini iliyotolewa hailingani na uhalisia wa hali ilivyo Tanzania kwa kuwa vyama vinaruhusiwa kufanya siasa kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi.
Aidha, amesema changamoto ya haki za binadamu zipo katika nchi zote, zinazonyoosha vidole na zinazonyoshewa vidole, na Tanzania inahakikisha haki za binadamu zinalindwa.