Taasisi ya Mahusiano ya Umma Tanzania (IPRT) imehitimisha mafunzo ya siku Tano ambayo yalianza octoba mbili hadi octoba sita mwaka huu kwa kundi la Maafisa na wakaguzi wanafunzi 953 wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA).
Akifunga mafunzo hayo Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Dkt. Lazaro Mambosasa amesema mafunzo hayo yakimkakati wa mawasiliano yamelenga kuwajengea uwezo wa kiutendaji maafisa na wakaguzi hao wanafunzi pindi watakapomaliza mafunzo yao Kwenda kutoa huduma bora kwa wananchi.
Dkt Mambosas ameongeza kuwa kumekuwepo dhana hasi katika mawasiliano baina ya Jeshi hilo na wananchi huku akiwataka maafisa hao Kwenda kubadilisha dhana hiyo ya mawasiliano yasiyo mazuri ambapo amewataka maafisa hao wanafunzi kuyapokea mafunzo hayo ambayo yataleta tija kiuchumi kwa watanzania pale watakapoweza kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika maeneo tofauti tofauti hapa nchini.
Kwa upande wake Mkurungezi wa Taasisi ya Mahusiano ya Umma Tanzania (IPRT) Dkt. Gabriel Nderumaki amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwaongezea uwezo wa mawasiliano ya kimkakati ambapo amebainisha kuwa Taassisi hiyo itaendelea kushirikiana na Jeshi hilo katika kuwaongezea uwezo wa kimawasiliano.
Nae Mratibu wa mafunzo kutoka taasisi ya Mahusiano ya Umma Tanzania IPRT Bi. Elizabeth Wachuka ameseama jumla ya mawasilisho katika mafunzo hayo yalikuwa ishirini na sita ambapo yaligawanywa katika makundi matatu ambayo ni mawasiliano, uongozi, dhana za uongozi huku akibainisha kuwa kundi lingine lilizingatia mafunzo ya Jeshi la Polisi yaliyotolewa na maafisa wastaafu wa Jeshi la Polisi.