Kutana na Dr Ipyana ambaye ni Daktari wa binadamu ambapo ameiambia AyoTV na millardayo.com kuwa kwa sasa anafanya udaktari kwa asilimia 20 na 80 anafanya muziki wa injili na yuko mbioni kabisa kuacha kazi hiyo ili afanye muziki wa Injili kwa asilimia 100.
‘Mungu ananilazimisha kubaki kwenye game hata kama sitaki, ndani ya kuacha udaktari huo mwaka nimepata vitu ambavyo sijawahi kuvipata ndani ya udaktari, ishu sio udaktari, nimepitishiwa magari kama matatu wakati siko kwenye kazi, concert niliyoifanya ni zaidi ya MILIONI 40, nimeenda South Africa, nimekaa siku 21 wakati sina mshahara wa Udaktari, Mungu ananiambia unaweza ukawa bado vizuri zaidi kuliko ulivyokuwa daktari’-Dr. Ipyana
Unaweza kutazama kila alichozungumza Dr. Ipyana kwa kubonyeza play hapa chini
BREAKING: Ugonjwa wa kutisha usio na tiba uliosababisha kifo cha Daktari JKCI, Bonyeza play hapa chini kuitazama