Shughuli ya upigaji kura unaendelea nchini Iran wakati nchi hiyo ikifanya uchaguzi wake wa kwanza tangu maandamano ya 2022 ya kupinga serikali.
Uchaguzi wa Ijumaa unaonekana kama mtihani muhimu wa uhalali na uungwaji mkono wa kitaifa kwa uongozi wa Iran.
Hali ya kutojali miongoni mwa wapiga imeongezeka kufuatia kipindi cha machafuko baada ya kifo cha msichana mdogo aliyezuiliwa na polisi wa maadili kwa kuvalia hijabu “inavyostahili”.
Zaidi ya watu milioni 61.2 wanatarajiwa kupiga kura. Chaguzi mbili tofauti zinafanyika Ijumaa: moja ya kuwachagua wabunge wafuatao, na mwingine kuwachagua wajumbe wa Bunge la Wataalamu.
Baraza hilo linamchagua na kumsimamia kiongozi mkuu na kamanda mkuu wa Iran, kiongozi mkuu – ambaye hufanya maamuzi muhimu kuhusu masuala muhimu kwa wapiga kura, kama vile uhuru wa kijamii na hali ya kiuchumi.
Siku ya Alhamisi, Kiongozi Mkuu wa kidini Ayatollah Ali Khamenei – ambaye ameshikilia wadhifa huo kwa zaidi ya miongo mitatu – aliwahimiza Wiran kutitokeza kwa wingi kupiga kura.
Kutopiga kura “hakuwezi kutatua chochote”, alisema.