Moja kati ya Habari iliyokamata headlines duniani ni pamoja na kusambaa kwa video ikionyesha tukio lililotokea katika duka moja kwenye mji wa Shandiz nchini Iran ambapo mwanaume mmoja aliwashambulia wanawake wawili waliokuwa ndani ya duka, baada ya kuona wanawake hao wawili walikuwa hawajavaa hijab, alinyakua beseni la mtindi na kuwamwagia vichwani mwao na kuwapiga wanawake wote wawili kichwani, baada ya hapo video inaonyesha mfanyakazi wa kwenye duka hilo akimwondoa mshukiwa dukani humo.
Wanawake hao wawili kutokea nchini Iran walikamatwa na kutiwa kizuizini baada ya mwanaume huyo kuwarushia mtindi kwa kutovaa hijab, kulingana na video na ripoti iliyochapishwa na Shirika la Habari la Mizan, vyombo vya habari vya serikali kwa mahakama ya Iran na mwanaume huyo pia amekamatwa kwa kuvuruga utulivu wa umma.
Wanawake wa kutokea Iran wapo hatarini kukamatwa kwa kutofunika nywele zao, wengi wamekuwa wakikaidi kanuni ya mavazi ya lazima kama sehemu ya maandamano yaliyofuatia kifo cha msichana aliyekuwa kizuizini ambae alidaiwa kukiuka sheria za hijab. Mwanzoni mwa wiki hii wanawake wengi wamepinga kitendo hichi hususani kwenye mitandao ya kijamii, huku Rais wa Iran akisisitika kuwa kutokuvaa hijab ni ukikwaji wa sheria na wanawake hao wanapaswa kuadhibiwa.