Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa wito wa kuchukuliwa hatua za “dharura” za kimataifa kwa lengo la kusimamisha vita vinavyoendelea vya utawala wa Israel vya mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza.
Akizungumza siku ya Jumatatu, msemaji Esmaeil Baghaei aliweka utepetevu wa taasisi za kimataifa, ikiwa ni pamoja na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, katika kukabiliana na mauaji ya kimbari kuwa ni uungaji mkono kamili wa Marekani kwa utawala huo.
Hata hivyo, alishutumu hali hiyo kama “ya aibu,” akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka kukomesha vita na kuwafungulia mashitaka na kuwaadhibu maafisa wa Israel kwa kutekeleza uhalifu wa kutisha.
Msemaji huyo amekariri hati za kukamatwa ambazo zilitolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai dhidi ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wa zamani wa masuala ya kijeshi wa utawala huo Yoav Gallant mwezi uliopita kutokana na jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu.
Alitaja wajibu wa mataifa ambayo ni sehemu ya sheria ya mahakama ya kutekeleza vibali, huku akisisitiza wajibu wa mataifa yote chini ya sheria ya kimataifa kuhakikisha kuheshimiwa kwa sheria ya kimataifa ya kibinadamu na kupiga marufuku mauaji ya kimbari.