Iran imetoa onyo juu ya vita vinavyoendelea vya Israel na Hamas kwani ilisema kuwa kiwango cha mateso ya raia bila shaka kitasababisha kupanuka kwa mzozo huo.
Haya yanajiri baada ya maafisa wa Gaza kuripoti mashambulizi ya anga ya Israel kwenye au karibu na hospitali kadhaa katika eneo la Palestina. Maoni hayo yametolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian.
“Kutokana na kupanuka kwa makali ya vita dhidi ya wakaazi wa raia wa Gaza, upanuzi wa wigo wa vita umekuwa jambo lisiloepukika,” Amir-Abdollahian alimwambia mwenzake wa Qatar Sheikh Mohammed Bin Abdulrahman Al Thani Alhamisi usiku.
Jeshi la Israel lilisema Ijumaa lilishambulia shirika moja nchini Syria ambalo lilikuwa nyuma ya ajali ya ndege isiyo na rubani katika shule moja kusini mwa Israel siku moja kabla.
“Katika kukabiliana na UAV (drone) kutoka Syria ambayo iligonga shule huko Eilat, IDF ilipiga shirika lililofanya shambulio hilo,” jeshi la Israeli lilisema katika chapisho kwenye X, zamani ikijulikana kama Twitter.