Iran inaandaa operesheni kali kabla ya kuadhimisha mwaka mmoja wa kifo cha Mahsa Amini, ikiwakamata watu mashuhuri, wanakampeni na jamaa za wale waliouawa na vikosi vya usalama katika maandamano mwaka jana, wanaharakati wanasema
Maandamano hayo sasa kwa kiasi kikubwa yamepungua, licha ya milipuko ya hapa na pale, baada ya msako mkali ambao ulishuhudia maelfu wakizuiliwa, kulingana na Umoja wa Mataifa, na mamia kuuawa kwa kupigwa risasi na vikosi vya usalama, kulingana na wanaharakati.
Lakini wanaharakati nje ya Iran wanasema mamlaka inafahamu vyema hatari kwamba maadhimisho hayo yanaweza kusababisha maandamano zaidi na kusema vikosi vya usalama vimeongeza ukandamizaji ili kuzuia marudio ya matukio ya vuli iliyopita.
Waliokamatwa mwezi huu ni pamoja na mwimbaji maarufu Mehdi Yarrahi baada ya kutoa wimbo akiwataka wanawake wavue hijabu zao kinyume na sheria.
Wanaharakati 11 wa haki za wanawake walizuiliwa katika jimbo la Gilan, mojawapo ya maeneo ambayo yalikuwa yanafanyika maandamano mwaka jana, kulingana na Shirika la Habari la Wanaharakati wa Haki za Kibinadamu (HRANA).
Wakati huo huo, Amnesty International imesema familia za watu waliouawa katika ukandamizaji wa harakati hiyo zimekabiliwa na “kukamatwa kiholela na kuwekwa kizuizini” katika harakati za kutekeleza “ukimya na kutokujali” juu ya hatima ya wapendwa wao.
Wakati huo huo, Haki za Kibinadamu za Iran yenye makao yake Norway, zimesema watu 486 wamenyongwa nchini Iran mwaka huu, huku matumizi ya adhabu ya kifo yakilenga “kuzua hofu katika jamii na kuzuia maandamano zaidi”.
Wakati wanaume saba wamenyongwa katika kesi zinazohusiana na maandamano, na kusababisha kilio cha kimataifa, wengi wa wale walionyongwa wanatiwa hatiani kwa makosa ya dawa za kulevya na mauaji na “wahasiriwa wa bei ya chini wa mashine ya mauaji ya jamhuri ya Kiislamu”, iliongeza.