Baraza la Usalama la Taifa la Iran limesitisha utekelezaji wa “sheria ya hijabu na usafi wa kimwili” yenye utata, ambayo ilikuwa ianze kutumika siku ya Ijumaa.
Rais Massoud Pezeshkian aliita sheria hiyo “ya utata na inayohitaji marekebisho”, akiashiria nia yake ya kutathmini upya hatua zake.
Sheria mpya iliyopendekezwa – ambayo ingeleta adhabu kali zaidi kwa wanawake na wasichana kwa kufichua nywele zao, mapajani au miguu ya chini – ilikuwa imekosolewa vikali na wanaharakati wa haki.
Kanuni kali za mavazi zilizowekwa kwa wanawake na wasichana, ambazo zimechukuliwa kama kipaumbele cha usalama wa taifa na watawala wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa miongo kadhaa, hapo awali zilizusha maandamano.