Serekali ya Iran imewakamata watu 28 wanao husishwa na kundi la Islamic State kwa kupanga shambulizi wakati wa maadhimisho ya maandamano ya mwaka jana mjini Tehran wizara ya ujasusi imesema Jumapili.
Maandamano yalizuka baada ya kifo cha Mahsa Amini aliyekuwa mikononi mwa polisi Septemba 16, 2022, binti huyo alikuwa na umri wa miaka 22 mwenye asili ya Kikurdi na alikamatwa kwa shutuma za kukiuka sheria za mavazi za Jamuhuri hiyo ya kislamu.
Wizara imesema katika siku za karibuni mfululizo wa oparesheni kali katika majimbo ya Teheran, Alborz, na Azerbaijan magharibi, vituo kadhaa vya magaidi na nyumba zimeshambuliwa ambapo wanachama 28 wa mtandao huo wa kigaidi 28.
Wizara ya ujajusi pia imesema maafisa wawili wa usalama walijeruhiwa wakati wa oparesheni ya ukamataji watu hao, na idadi kadhaa ya mabomu, bunduki, koti za kuvalia mabomu ya kujitoa muhanga na vifaa vya mawasiliano vilikamatwa.
Maandamano ya miezi kadhaa yalishuhudia mamia ya watu wakiuawa, wakiwemo makumi ya maafisa wa usalama, katika kile Tehran ilichokiita “machafuko” yaliyochochewa na serikali za kigeni na “vyombo vya habari vya uhasama”.
Siku ya Alhamisi, mahakama ilimhukumu kifo mwanachama wa kundi la Tajik IS aliyepatikana na hatia kwa shambulio baya la bunduki kwenye hekalu la Waislamu wa madhehebu ya Shia mwezi Agosti.