Iran imewakamata watu 35 kuhusiana na mashambulizi ya Januari 3 katika mji wa Kerman kusini-mashariki, wizara yake ya upelelezi imesema.
Ikinukuu shirika la habari la Tasnim, Reuters inaripoti kuwa wizara hiyo ilisema imemtambua mmoja wa washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga kuwa ni raia wa Tajikistan, ambaye aliingia Iran kinyume cha sheria tarehe 19 Disemba.
Taarifa zaidi zitatolewa baadaye kuhusu mshambuliaji wa pili wa kujitoa mhanga, wizara hiyo ilisema, ikiongeza kuwa kukamatwa kwa watu hao kumetekelezwa katika mikoa kadhaa ya Iran.
Islamic State ilidai kuhusika na shambulio hilo lililoua karibu watu 100 na kujeruhi 284 katika hafla ya kumbukumbu ya kifo cha kamanda mkuu wa Walinzi wa Mapinduzi Qassem Suleimani.