Mamlaka ya Iran imewakamata washukiwa wengine wanne baada ya kumzuilia mtu mmoja aliyekuwa na bunduki katika mauaji ya angalau mtu mmoja katika madhabahu ya Waislamu wa madhehebu ya Shia, vyombo vya habari vya serikali viliripoti Jumatatu.
Shambulio hilo lilitokea chini ya mwaka mmoja baada ya shambulio kama hilo kwenye eneo takatifu la Shah Cheragh huko Shiraz, mji mkuu wa mkoa wa Fars kusini mwa Iran.
Shirika rasmi la habari la IRNA limemnukuu jaji mkuu wa jimbo la Fars Kazem Mousavi akisema kuwa “washukiwa wanne hadi sasa wamekamatwa kwa kuhusishwa na shambulio hilo.”
Wanne hao ni pamoja na mshambuliaji ambaye kukamatwa kwake kulitangazwa Jumapili usiku na kamanda wa Fars wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Yadollah Bouali, ambaye alizungumza kwenye TV ya serikali.
Mbali na kifo hicho, watu wanane walijeruhiwa, IRNA iliripoti.
Hakukuwa na madai ya kuhusika mara moja lakini gavana wa jimbo la Fars Mohammad Hadi Imanieh alilaumu kundi la Islamic State.
Aliambia runinga ya serikali kwamba mshambuliaji alitaka “kulipiza kisasi kwa kunyongwa kwa magaidi wawili” waliopatikana na hatia ya kutekeleza shambulio kama hilo mwaka jana.