Kwa muda mrefu sasa hivi ni Ndege ndogo tu zimekua zikitua kwenye uwanja wa Ndege wa Iringa na hiyo haimpendezi Mkuu wa Mkoa Ally Hapi ambae ni juzijuzi tu aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa huo, lengo lake ni kuibadilisha na kuipandisha juu zaidi Iringa.
Kwenye ziara yake anayopita kwenye maeneo mbalimbali Iringa, RC Hapi ametangaza good news ya Ndege kubwa za Bombadier za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuanza kutua Iringa hivi karibuni.
Amesema “Juzi nilipokua Dodoma nimezungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Ndege Tanzania, muda sio mrefu Bombadier zitaanza kutua Iringa na Bombadier sio ghali“
Akaongeza “Wafanyabiashara wengi wanaogopa kuja kuwekeza Iringa kwasababu Mtu mwenye fedha sasa havi hayuko tayari kusafiri saa 5, 6 au 7 barabarani anaendesha gari kuja Iringa, Watu wanataka waruke watue, asubuhi yupo Iringa jioni analala DSM“
ULIPITWA: ALLY HAPI AAGIZA ASKARI WAONDOKE NA MENEJA WA BENKI NA MWANASHERIA.. BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA