Waziri wa ulinzi wa Israel kwa mara ya kwanza amekiri kuwa Israel ilimuua kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh mjini Tehran mwezi Julai.
Israel Katz alitoa maoni hayo katika hotuba yake akiahidi kuwalenga wakuu wa vuguvugu la Houthi linaloungwa mkono na Iran nchini Yemen, ambalo limekuwa likirusha makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya Israel.
Haniyeh aliuawa katika jengo alimokuwa akiishi katika mji mkuu wa Iran katika shambulizi linalohusishwa na Israel.
Kando, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema baadhi ya mafanikio yamefikiwa katika kukubaliana kusitisha mapigano huko Gaza na Hamas, lakini hakuweza kutoa ratiba ya lini makubaliano yatafikiwa.
Yeyote atakayeinua mkono dhidi ya Israeli atakatwa mkono wake, na mkono mrefu wa IDF (jeshi la Israeli) utampiga na kumwajibisha,” Katz alisema, kulingana na taarifa iliyotolewa na wizara alisema