Israel inasema imewauwa zaidi ya wanamgambo 10,000 wa Kipalestina lakini haijatoa ushahidi wowote wa kuhesabiwa kwake. Jeshi linasema linajaribu kuzuia kuwadhuru raia na linalaumu idadi kubwa ya vifo kwa Hamas kwa sababu kundi la wanamgambo wanapigana katika vitongoji vyenye makazi ya watu.
Jeshi linasema wanajeshi wake 236 wameuawa tangu kuanza kwa mashambulizi ya ardhini mwishoni mwa Oktoba.
Siku ya Jumapili, Benny Gantz, mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Vita la watu watatu la Netanyahu, alionya kwamba mashambulio hayo yataenea hadi Rafah ikiwa mateka hawataachiliwa ifikapo mwanzo wa mwezi mtukufu wa Waislamu wa Ramadhani, unaotarajiwa karibu Machi 10.
Tayari, vita hivyo vimewafurusha karibu asilimia 80 ya Wapalestina huko Gaza kutoka makwao na kuwaacha robo ya watu wakiwa na njaa, kulingana na maafisa wa Umoja wa Mataifa.
Marekani inasema bado inashinikiza kusitishwa kwa mapigano na kuachiliwa kwa mateka, na kwamba ingepinga azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusitishwa mara moja kwa mapigano kwa sababu linakinzana na juhudi hizo.