Israel na kundi la wapiganaji wa Palestina Hamas wameibua wasiwasi juu ya orodha ya mateka wa Israel na wafungwa wa Kipalestina wanaotazamiwa kuachiliwa siku ya Jumatatu, afisa aliyearifiwa kuhusu suala hilo aliambia Reuters.
Afisa huyo ameongeza kuwa wapatanishi wa Qatar wanafanya kazi na Israel na Hamas kutatua masuala na kuepuka ucheleweshaji.
“Kuna suala kidogo katika orodha za leo,wanafanya kazi na pande zote mbili ili kutatua na kuepuka ucheleweshaji,” afisa huyo alisema.
Katika siku tatu zilizopita za mapatano hayo Israel iliwasilisha majina ya wanawake na vijana wa Kipalestina ambayo ingewaachia kutoka jela na Hamas ingewasilisha majina ya mateka raia wa Israel ambayo ingewaachia angalau saa 12 kabla ya kuachiliwa.