Nchi ya Israel imekuwa namba moja Duniani kwa kutoa bei rahisi za Bando za Internent mwaka huu ambapo GB 1 inagharimu USD 0.05 (Tsh. 116.19) kwa mujibu wa takwimu za mtandao wa Cable wa Uingereza, Israel ilikuwa nafasi ya Pili mwaka jana.
India imeishangaza Dunia kwa kutoka kwenye nafasi ya kwanza mwaka jana kwa bei nafuu ya Bando Duniani hadi nafasi ya 28 ambapo GB 1 kwa sasa inagharimu USD 0.68.
Kwenye tano bora ya dunia ya bei rahisi ya bando ipo pia Sudan (USD 0.27), kwa Afrika Mashariki Tanzania imetajwa kuwa ni Nchi ya kwanza kwa mwaka wa pili mfululizo ambapo bei ya bando zake za internet ni nafuu kwa mujibu wa takwimu za mtandao huo wa Cable wa Uingereza.
Kwenye ripoti hiyo yenye takwimu za dunia nzima ambazo zimekusanywa kuanzia December 08 2020 hadi February 25,2021 inaonesha kuwa Tanzania ina bando rahisi ambayo ni USD 0.75 (Tsh. 1,742.81) kwa GB moja ikifuatiwa na Rwanda (USD 1.25), Uganda (USD 1.56) na Burundi (USD 2.10), Kenya ilikuwa ya pili mwaka jana ambapo bando iligharimu USD 1.04 kwa kila GB lakini kwa mwaka huu gharama zimepanda na kufikia USD 2.25.
ULIPITWA? HII NI TATHMINI YA MWALIMU KASHASHA KWA SIMBA HII