Israel imekanusha kwa hasira madai kwamba imetishia usalama wa waziri wa Afrika Kusini, na kwa upande wake imemshutumu kwa “kashfa ya damu” na “kutumika kama mrengo wa kisheria” wa Hamas.
Uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulidorora mwezi uliopita, wakati Afrika Kusini ilipowasilisha kesi dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ikiishutumu Israel kwa kufanya mauaji ya kimbari huko Gaza – mashtaka ambayo imeyakataa
Awali Waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Afrika Kusini Naledi Pandor aliiituhumu idara ya ujasusi ya Israeli kwa kile anachodai kuwa idara hiyo imekuwa ikimtishia kufuatia hatua yake ya kuwasilisha kesi katika mahakama ya ICJ kuhusu kinachoendelea Gaza.
Akizungumza na majarida ya The Mail na The Guardian siku ya Alhamis, waziri huyo ameeleza kwamba ana wasiwasi kuhusu maisha yake na familia yake baada yake kulengwa kwenye mitandao ya kijamii.
Kwa mujibu wa waziri huyo, tayari ametoa taarifa kwa mwenzake wa polisi nchini Afrika Kusini Bheki Cele kumuongezea ulinzi baada ya kupokea kile anchodai ni kupokea taarifa za vitisho.