Takriban watu 242 walichukuliwa mateka wakati wa mashambulizi ya Hamas, jeshi la Israel limesema.
Mara ya mwisho ilisema watu 240 walitekwa nyara, huku Hamas ikiwaachilia raia wanne tangu tarehe 7 Oktoba.
Wengi wanafikiriwa kufichwa kwenye mtandao mkubwa wa chini ya ardhi wa kundi hilo huko Gaza.
Takriban Wapalestina 195 waliuawa baada ya mashambulizi mawili ya Israel kwenye kambi kubwa zaidi ya wakimbizi ya Gaza siku ya Jumanne na Jumatano, ilisema ofisi ya vyombo vya habari vya serikali inayoongozwa na Hamas katika taarifa.
Kundi la wanamgambo wa Kipalestina pia lilisema kuwa takriban 120 bado hawajulikani waliko chini ya vifusi, na takriban 777 zaidi walijeruhiwa.