Agape Moses Ni msichana mwenye umri wa miaka 19 anayeishi kijiji cha ngurdoto wilayani Arumeru mkoani Arusha, ambaye amesaidia kijiji chake kupata maji.umeme pamoja na darasa la Computer kwenye kijiji chake baada yakufanya vizuri shuleni nakupata wafadhili nakuamua kumsaidia kufanya hivyo pamoja na kufadhiliwa kusoma bure hadi kidato cha sita
Agape akizungumza kwenye Exclusive na Ayo tv pamoja na millardayo.com amesema anaugua ugonjwa wa viungo ambapo kwenye familia yake yenye watoto sita wadogo zake wawili wote ni walemavu ambapo mdogo wake Riziki anaulemavu lakini amewashangaza watu baada yakusoma madarasa matano kwa mwezi mmoja kutokana nakuwa na uwezo mkubwa wa elimu.
‘kuna muda nashindwa kusimama naanguka nakuumia ila namshukuru Mungu,mimi nimepata ufadhili ila nina mdogo wangu ambaye anatumia miguu ya bandia na imeishaisha muda wake kama watatokea watu wakatusaidia nitashukuru”-Agape
Moses Ayo ambaye ni baba wa watoto hao amesema amebahatika kupata watoto sita lakini watoto wake watatu ni walemavu lakini ulemavu wao haujaathiri akili na anawapenda sana.