Kwa Sheria za kazi hapa Tanzania ukikutwa unafanya baadhi ya vitu kama, kuvuta sigara au kunywa pombe ukiwa kazini inaweza kukusababishia matatizo makubwa ikiwemo kufukuzwa kazi… lakini hii kwa wenzetu wa Italiano imekaa aje?
Unaambiwa kwa wenzetu wa Italiano ukikutwa unavuta bangi kwenye muda wa mapumziko hiyo ni issue kubwa sana na pengine itakugharimu kazi yako, lakini sio kwa kutazama picha za utupu kwenye muda wa mapumziko kazini kwani kitendo hicho hakitaathiri kwa vyovyote vile utendaji wako wa kazi kama vile ambavyo bangi ina uwezo mkubwa wa kuathiri utendaji kazi wa mtu kushuka ofisini!
Yes! Kama ulikuwa hujaipata hiyo basi ikufikie mtu wangu… Kwa mujibu wa mtandao wa Complex wa Marekani, Mahakama ya Juu ya Italy imesema kwamba unaweza kufukuzwa kazi kama ukikutwa unavuta bangi muda wa mapumziko kwani kitendo hicho kinaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kusababisha utendaji kazi wa mtu kushuka, lakini utazamaji wa picha za utupu hauathiri utendaji wa kazi kwa kiasi chochote kile bali itategemea na mtu mwenyewe.
Mahakama hiyo iliendelea kusema kama mtu ataamua kutumia muda wake wa mapumziko kuangalia picha za utupu kwenye computer za ofisi, basi ofisi haitakuwa na mamlaka yoyote yale kuingilia muda huo kwani ni muda binafsi wa mfanyakazi, lakini kama mfanyakazi angekuwa anautumia muda huo kufanya mauzo (biashara) ya picha hizo ofisini basi hapo ingekuwa kosa ambalo lingeweza kugharimu mtu kazi yake lakini sio tofauti na hapo.
Maamuzi hayo yalitokana na kesi ya Rufaa iliyofikishwa Mahakamani huko na mfanyakazi wa kampuni moja ya kutengeneza magari huko Italy kwa madai ya kuwa alifukuzwa kazi kinyume na Sheria pamoja na Mkataba wake wa kazi uliosema kuwa “muda wa mapumziko, kila mtu ana uhuru wa kufanya shughuli zake binafsi…” kutokana na muda uliyotolewa na kampuni hiyo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE