MSIMAMO WA TZ KUHUSU MAHAKAMA YA ICC
Serikali ya Tanzania imesema msimamo wake uko palepale sawasawa na msimamo wa nchi za Afrika ambapo kwa pamoja wanapingana na utaratibu wa uendeshaji wa kesi za Mahakama ya ICC licha ya Mahakama hiyo kumfutia mashtaka Rais Uhuru Kenyatta.
Akizungumza kuhusu msimamo huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema; “lakini bado tunashikilia msimamo wetu ambao mwezi Januari tutautoa kwamba wala hakuna sababu ya kudhalilisha viongozi wa Afrika na kuwanyanyasa kama viongozi ambao ni watu tu wa kawaida au wahalifu mpaka mkawaburuza kuwapeleka the Hague, hii kwakweli sisi hatuikubali… Wanatenda haki lakini mchakato wenyewe wa kutenda haki unadhalilisha viongozi…”
MAJAMBAZI WAWILI WAUAWA TANGA
Watu wawili wanaodhaniwa kuwa majambazi wameuawa Tanga baada ya kuvamia kiwanda cha kusindika Chokaa na kufanya jaribio la kupora fedha kiasi cha milioni 100 kutoka kwa Mhasibu wa Kiwanda hicho.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Juma Ndaki amesema; “majambazi hao waliouawa ni Timoth Charles mkazi wa Mkwajuni Dar es Salaam, pamoja na Mwinyimkuu Khamis mkazi wa Chanika, Dar es Salaam…”
Majambazi hao walikuwa wanne lakini wawili kati yao waliokuwa wamebaki nje walikimbia baada ya kushtuka kuwa wenzao wamebainika.
MELI YA Mv MAPINDUZI II KUWASILI Z’BAR
Meli ya Mv Mapinduzi II inatarajiwa kuwasili mapema mwezi Januari visiwani Zanzibar kwa ajili ya majaribio baada ya kununuliwa kutoka Korea Kusini ilipokuwa inaundwa.
Meli hiyo ambayo imenunuliwa na Serikali ya Zanzibar kutokana na pato la kodi ina uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 200 za mizigo.
Meli hiyo imegharimu kiasi cha dola milioni 30 mpaka kukamilika.
Nimekuwekea hapa habari hiyo niliyokurekodia kutoka ITV, unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook