Leo ndio mwisho wa Matangazo ya TV kwa Mfumo wa Analogy Tanzania
Wakati TZ ikitangaza kuzima Mitambo ya kurushia Matangazo ya Analogy mwaka 2012 ilkuwa ishu ambayo watu wengi hawakukubaliana nayo, ilikuwa kama watu wamewahishwa kuingia kwenye mfumo huo mpya wa Matangazo, leo iko stori nyingine kutoka TCRA ambapo wametangaza rasmi kwamba leo ndio siku ya mwisho kwa Matangazo ya Analogy kuruka Tanzania.
Wabunge na Ishu ya Bidhaa toka Nje ya TZ.
Wabunge wameilalamikia Serikali kwa kushindwa kudhibiti uingizwaji wa bidhaa nyingi toka nje ya TZ kitu ambacho kinasababisha kushuka kwa thamani ya shilingi.. Wabunge hao wamesema bidhaa ndogondogo kama soksi, vitambaa vya mikononi, hata dodoki la kuogea vinaagizwa toka China badala ya kuviwezesha Viwanda vya ndani viweze kuzalisha bidhaa hizo.
Ajali ya moto Msasani Dar.
Maduka matatu yameteketea Msasani Dar usiku wa kuamkia leo, Zimamoto walifika na kuuzima moto huo japo wanalaumiwa kwa kuchelewa kufika kuuzima moto huo.
Ndani ya nyumba ambako kuna maduka hayo anaishi bibi mmoja ambae amesema baada ya kushtuliwa kwamba kuna moto alilazimika kutambaa ili kujiokoa kwa vile ana tatizo la miguu.
Chanzo cha moto huo kimetajwa kuwa ni shoti ya umeme.
Stori zote ziko kwenye hii sauti toka kwenye Habari ya ITV June 17 2015.