Katika taarifa kubwa mbili zilizoripotiwa na kituo cha ITV kwenye habari za saa siku ya leo Desemba 02, ni kuhusu kile kilichosemwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya PAC na Dk. Khamis Kigwangala kuhusiana na wananchi kukosa imani na Serikali na habari nyingine ni kuhusu Kikao cha Bunge la Vijana Dodoma.
Dk. Kigwangwala: Wananchi wanakosa imani na Serikali
Tabia ya Serikali kutochukua hatua kali za kisheria kwa viongozi wanaobainika kuchukua mali ya umma inawafanya wananchi kukosa imani na Serikali yao na pengine kusababisha kutoweka kwa amani kwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuvumilia shida wakati anaona watu wachache wakigawana mali na kuendelea na nyadhifa zao.
Akizungumza hayo Kigwangala amesema; “…Haya hayakubaliki na hatuwezi kukubali kundi la watu wachache kutoka kizazi kingine wamepewa dhamananchi imewapa heshima kubwa wanaendelea kuiba wakati na sisi tupo, waadilifu tuendelee kutazama jambo hilo tumesema hapana hatutoruhusu mtu atumie pesa zetu, halafu afukuzwe tu kazi yaishie hapo aende kutanua huko mjini nasema aendelee kutumia pesa zake … aende akaishi kwa raha huko nje…“
Kikao cha Bunge la Vijana Dodoma
Katika taarifa nyingine ITV imeripoti kuanza kwa Bunge la Vijana ambapo, Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, limeandaa Bunge maalum la Vijana linalofanyika kwa mara ya kwanza chini ya Bunge la Tanzania mjini Dodoma kwa siku tatu.
Bunge hilo linajumuisha vijana 150 kutoka vyuo vikuu nchini ili kuwajengea uwezo wa kushiriki kikamilifu katika masuala ya Kibunge na Siasa kwa kutambua wao ni Viongozi wa kesho.
Akiwa katika eneo la viwanja vya Bunge, mmoja ya vijana hao amesema “… Kwanza kabisa kwa upande wangu wa Serikali nzima ni kufuata kanuni ambazo zimewekwa kuendesha Bunge hili la Vijana, pili ni kufuata yale ambayo kambi nzima ya Serikali imepanga kusimamia kile ambacho kinatupeleka katika mchakato mzima na mswada mzima wa Sheria ambayo tunayotaka kuitunga…”
Nimekuwekea hapa sauti ya taarifa hiyo, unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play hapa.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook