Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe leo February 22, 2018 anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi cha Mgeta wilayani Mvomero, Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya mahojiano.
Zitto yupo katika ziara ya mikoa mbalimbali kwa ajili ya kukagua na kuimarisha uhai wa chama hicho.
Akizungumza na millardayo.com na AyoTV Katibu Kamati ya Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa ACT Wazalendo Ado Shaibu amesema mpaka sasa bado yupo anashikiliwa na Polisi hawajui ni kosa gani ambalo Zitto Kabwe limefanya akamatwe
Nae Wakili wa Zitto Kabwe, Emmanuel Lazarus Mvula amesema jalada la mashataka dhidi yake limefunguliwa katika kituo cha Polisi Mgeta.
“Hivi Sasa saa 3.30 usiku ndugu Zitto amechukuliwa na OC-CID na polisi wenye silaha anapelekwa Kituo cha Polisi cha Wilaya, cha Dakawa ili kuandika maelezo kwasababu hakuna umeme katika kituo cha Polisi Mgeta” -Zitto Kabwe
JPM kwenye Mkutano wa 19 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki