Kinyang’anyiro cha Udiwani katika Kata ya Reli iliyopo Halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani kimehitimishwa November 26, 2017 baada ya kupigwa kura na kuhesabiwa katika kata hiyo ambapo mgombea Genfried Mbunda wa CCM ametangazwa kuwa mshindi.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi James Tamba amesema mgombea wa CCM, Mbunda amepata ushindi kwa kura 422 ambazo ni sawa na 50.96% akimzidi mgombea wa CHADEMA Antony Sylvester Kwezi aliyepata kura 356 sawa na 42.99%.
Wagombea wengine katika uchaguzi huo walikuwa Mwajuma Hasani Ankoni wa ACT Wazalendo ambaye amepata kura 27 ambazo ni sawa na 3.26%, Mwomba P. Peter wa CUF aliyepata kura 21 sawa na 2.53% na mgombea wa NCCR-Mageuzi Yahaya Fundi aliyepata kura 2 sawa na 0.24%.
Jumla ya wapiga kura waliojiandikisha ni 2320 na waliojitokeza kupiga kura ni 842 ikiwa ni sawa na 36.29%.
Ulipitwa na hii? BREAKING: Agizo la Mbowe, CHADEMA yajitoa Uchaguzi wa Udiwani
CHADEMA kuhusu hali ilivyo kwenye uchaguzi wa madiwani