Kama ulikuwa unafikiri Ivo Mapunda mpira ndio ilikuwa kazi yake rasmi ya kwanza basi utakuwa unakosea, Ivo Mapunda ambao wengi tumemfahamu kupitia kipaji chake cha soka na umairi wake wa kusimama imara katika milingoni mitatu Uwanjani, ametupa historia yake fupi ya kitafutaji katika maisha na kazi gani alikuwa anaifanya.
Ivo ambaye amekuwa akiingia katika headlines za vyombo vya habari tofauti tofauti kwa hivi karibuni kufuatia ule uvumi uliokuwa ukizungumzwa kuwa amegomea kusaini mkataba na Simba licha ya kuwa ameshapewa fedha za usajili, team ya millardayo.com ilimtafuta ili kufanya naye exclusive interview na kuwapa watu nafasi ya kumfahamu zaidi.
Licha ya kumuona uwanjani Ivo kumbe alikuwa askari magereza na alikuwa akicheza klabu ya jeshi la magereza kabla ya kuhamia Moro United kwa dau nono na kumfanya avue gwanda za magereza na kuhamia Moro United halafu Yanga.
“Nimecheza Prisons huku nikiwa mfanyakazi wa jeshi la magereza kwa miaka sita nilikuwa na cheo cha copro baada ya hapo nikajiunga Moro United, mpira ndio kipaji changu Mungu amenipatia baada ya kuona maisha ya askari ni kazi ambayo ilikuwa inanipa shida, nikaona wacha niendelee na mpira dau nililokuwa nimelipwa kipindi hicho na Moro United nikaona inatosha kabisa mimi kuacha kazi ya uaskari” >>>Ivo Mapunda
Hii ni sauti ya Ivo unaweza msikiliza hapa
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos