Raia wa Ivory Coast jana walishiriki katika zoezi la kupiga kura ya kumchagua Rais ambapo Rais Alassane Ouattara anawania Madaraka kwa Awamu ya 3.
Inaelezwa, Wananchi wengi wana wasiwasi wa kutokea kwa ghasia na machafuko makubwa baada ya Kambi ya Upinzani kutoa wito wa kususiwa kwa Uchaguzi huo.
Watu 30 wameuwawa katika vurugu tangu mwezi Agosti, wakati Rais Ouattara alipotangaza kuwania Muhula wa Tatu, hatua ambayo Upinzani unasema unakiuka Katiba ya Nchi.
Ouattara amesema anagombea tena chini ya Katiba Mpya iliyoidhinishwa 2016, na anafanya hivyo kwa sababu Mgombea aliyechaguliwa na chama chake alifariki ghafla mwezi Julai.
LIVE: MAGUFULI ANAVYOKABIDHIWA CHETI CHA USHINDI, OFISI ZA NEC DODOMA