Kama wewe ni mmoja kati ya watu ambao umekua ukikutana na Chocolate inayotoka nje ya Nchi yenye nembo inayofananishwa na Chocolate ya Ivori Iringa ukahisi labda wamebadilisha muonekano wa nembo yao sasa Uongozi wa Kampuni ya IVORI IRINGA inayo majibu yake kwenye hizi sentensi 5 na inabidi uzingatie pia unapoenda dukani kununua.
1-Kuhakikisha kila bidhaa unayonunua ya IVORI ina Nembo Halisi ya IVORI yenye Herufi I mwanzoni na herufi I mwishoni.
isomeke IVORI CHOCOLATE na Sio IVORY CHOCOLATE
2-Bidhaa zetu zote zinatengenezwa TANZANIA,Tunajivunia Uzalendo wetu na ndio maana bidhaa zetu zote ni MADE IN TANZANIA .
3-Hakikisha kila Chocolate yetu unayoinunua ina Rangi ya kahawia ndani ya pakiti yake ikiwa na Ladha tamu ya maziwa ikitegenezewa na COCOA Halisi inayolimwa na Wakulima Nchini TANZANIA
4-Rangi ya kifungashio chakeni ya Njano iliyochanganywa na Rangi ya Zambarau.
5-Gharama zetu Elekezi ni Shilingi 1000 kwa Gram 40 na Shilingi 500 kwa Gram 20 na hatuna ujazo unaozid gram 40.
Iwapo kuna utofauti wa Bidhaa unayoiona na kuitilia shaka kampuni ya IVORI wanaomba sana uwasiliane naokwa sababu inabidi uwe Mjanja ili Usidanganyike Kununua Bidhaa Feki,Nunua Bidhaa Orijino Za Ivori Iringa, Epuka Kutapeliwa.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE