Siku chache zilizopita Mtanzania Omega Mwaikambo anayeishi Uingereza alihukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela kwa kupost kwenye Facebook mabaki ya mwili wa mtu aliyeungua moto kwenye ajali ya moto ulioteketeza ghorofa la Grenfell Tower.
Sheria inasemaje kuhusiana na tukio hilo? Majibu anayo Wakili wa kujitegemea na Mwanaharakati wa Haki za Binadamu Tanzania Jebra Kambole ambaye amekaa kwenye interview na Ayo TV na millardayo.com kufafanua zaidi juu ya tukio hilo kulingana na sheria.
>>>”Tanzania ipo sheria ya posta na mawasiliano ya mwaka 2010. Katika sheria hiyo kifungu namba 118 inakataza mtu kutuma picha au ujumbe inayooneka kuudhi, kushusha thamani ya mtu, kukera au kutisha.
“Kwa hiyo, sheria kama hiyo ipo na changamoto ambayo tunayo labda mimi niweze kusema unaweza kukuta Tanzania watu wanatuma na hawakamatwi na mambo yanaendelea kama yalivyo. Changamoto ambayo tunayo ni katika kusimamia hiyo sheria.” – Jebra Kambole.
Wakili Kambole amefafanua zaidi na unaweza kuplay VIDEO hii kumsikiliza zaidi!!
Kufuatia tukio la walemavu kupigwa mabomu ya machozi na Polisi, Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba amefunguka…unaweza kutazama VIDEO hii kwa kubonyeza PLAY kujua amesema nini juu ya tukio hilo!!!
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo